Simba yatangaza viingilio Kariakoo Derby

Joel JJ By Joel JJ
β€’
30 Oct 2023
Simba yatangaza viingilio Kariakoo Derby

Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ally ametangaza viingilio vya mchezo wa ligi kuu ya NBC kati ya Simba dhidi ya Yanga ambao utapigwa Jumapili, Novemba 05 katika uwanja wa Benjamin Mkapa

Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari mapema leo, Ahmed alisema Simba inahitaji ushindi katika mchezo huo, mashabiki wamekuwa silaha muhimu kwa Simba, Jumapili wanahitajika kwa wingi wao

"Ni mechi ambayo Wanasimba inabidi tujitoe muhanga ili kupata ushindi. Kila Mwanasimba ajue ana jukumu la kusaidia timu yake. Tukishinda siku hiyo shughuli itakuwa imeisha, itabaki shughuli ya kukamilisha ratiba ya msimu"

"Raha ya msiba waliaji wawe wengi, tunawaomba mashabiki wao waje uwanjani na wakae hadi mwishoni sio tukishawafunga wawahi kuondoka, wasubiri hadi mchezo uishe"

"Viingilio Mzunguko - Tsh. 5,000, Machungwa - Tsh. 10,000, VIP C - Tsh. 20,000, VIP B - Tsh. 30,000, VIP A - Tsh. 40,000 na Platinum - Tsh. 150,000," alisema Ahmed

Adha Ahmed amebainisha kuwa kikosi cha Simba kinatarajiwa kuingia kambini kesho Jumanne kwa ajili ya maandalizi ya mchezo huo

"Kikosi kitaingia kambini kesho Jumanne, kwa kawaida mechi za ndani huwa tunaingia siku tatu kabla ya mchezo lakini hii tunawahi. Tumeutolea macho mchezo huu kuhakikisha tunapata ushindi."

"Kocha wao ameshakuja kwenye mechi tatu hadi sasa na leo tunatangaza kumkaribisha kwenye mazoezi yetu yatakayofanyika Mo Simba Arena. Tunamualika rasmi aje siku yoyote anayotaka."

"Sisi hatuna jambo dogo hivyo tutafanya hamasa, ni mchezo wetu, tutautangaza tutakavyo tunajua watu watakuja lakini lazima tuichangamshe. Tutakuwa na wiki ya mchakamchaka wa kuaga kwao aage atarudi Jumatatu ya Novemba 6, 2023," alitamba Ahmed

ADVERTISE HERE

More Stories

Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
32m ago
READ MORE β†’
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
1h ago
READ MORE β†’
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
4h ago
READ MORE β†’
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
6h ago
READ MORE β†’
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
7h ago
READ MORE β†’
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
7h ago
READ MORE β†’
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
9h ago
READ MORE β†’
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
9h ago
READ MORE β†’
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
9h ago
READ MORE β†’
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
22h ago
READ MORE β†’