Transfer - International

Tetesi za soka Ulaya, Jumanne Oktoba 31 2023

Joel JJ By Joel JJ
β€’
31 Oct 2023
Tetesi za soka Ulaya, Jumanne Oktoba 31 2023

Real Madrid wako tayari kujadiliana na Chelsea kuhusu mkataba wa kudumu wa Kepa Arrizabalaga, lakini hawatalipa zaidi ya euro milioni 17.5 kwa kipa huyo Mhispania mwenye umri wa miaka 29 ambaye aliigharimu The Blues takriban euro milioni 71.6 miaka mitano iliyopita. (Sun)

Juventus huenda ikatumia mshahara uliookolewa kwa kiungo wa Ufaransa Paul Pogba, 30, kumpata kiungo wa Arsenal Thomas Partey, 30, katika mkataba wa mkopo mwezi Januari. Pogba anakabiliwa na adhabu ya kufungiwa kwa muda mrefu kutojihusisha na soka ambayo itasababisha kupunguzwa kwa mshahara kutoka kwa Juve. (Mirror)

Mkufunzi wa Arsenal Mikel Arteta ameripotiwa kuwaongeza viungo Martin Zubimendi, 24, wa Real Sociedad na Uhispania na Aurelien Tchouameni, 23, wa Real Madrid na Ufaransa kwenye orodha ya walengwa wa kuhama. (Calciomercato - kwa Kihispania)

Chelsea wana nia ya kumsajili kiungo wa kati wa Ujerumani Florian Wirtz kutoka Bayer Leverkusen huku Manchester City pia wakimtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20. (Express)

Chelsea ilituma maskauti kumtazama mlinda mlango wa Georgia na Valencia Giorgi Mamadashvili, 23, kwenye mechi ya timu hiyo ya Uhispania ugenini Granada Jumapili. (90 min)

Kocha wa The Blues Mauricio Pochettino pia anavutiwa na kipa wa Athletic Bilbao na Uhispania Unai Simon, 26. (Fichajes - kwa Kihispania)

Napoli wako tayari kufanya mazungumzo ya mkataba mpya na mshambuliaji wa Nigeria Victor Osimhen huku Liverpool wakihusishwa na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24. (Fichajes - kwa Kihispania)

Beki wa Chelsea na England Trevor Chalobah, 24, amevutiwa na Borussia Dortmund. (Sun)

Mshambuliaji wa kimataifa wa Uingereza Divin Mubama, 19, amekataa kuongezewa mkataba katika klabu ya West Ham ikiwa imesalia mwaka mmoja katika mkataba wake wa sasa. (the athletic- Usajili unahitajika)

BBC

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
4h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
4h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
4h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
8h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
11h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
12h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
12h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
13h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
14h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
15h ago
READ MORE β†’