Klabu ya Al Hilal ya Sudan imetangaza rasmi kutumia Uwanja wa Mkapa uliopo Dar es Salaam, Tanzania katika mechi za hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika
Al Hilal ipo kundi moja na timu za ES Tunis, Etoile Sportive du Sahel za Tunisia na Atletico Petroleos ya Angola
Kupitia akaunti yao rasmi ya Instagram wameishukuru TFF kwa kuwakubalia ombi lao la kutumia uwanja huo wenye uwezo wa kuingiza mashabiki 60,000
Al Hilal iliweka kambi nchini Morocco ikikimbia vita vinavyoendelea huko Sudan
Al Hilal imeungana na klabu za Simba na Yanga ambazo pia zinatumia uwanja wa Benjamin Mkapa katika mechi zao za ligi ya mabingwa hatua ya makundi



