Disemba 11 2023 tuzo za soka barani Afrika zinazotolewa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF)
Yanga imetajwa kuwa miongoni mwa klabu 10 zinazowania tuzo ya klabu bora ya mwaka barani Afrika kwa msimu wa 2022/23
Mabingwa hao wa ligi kuu ya NBC kwa misimu miwili mfululizo wakiwa wameshinda mataji yote ya ndani, wanachuana na vigogo wengine kama Al Ahly, Mamelodi Sundowns, Wydad Athletic, Raja Casablanca, Esperance, ASEC, USMA, CR Belouizdad na Marumo Gallants

Kushinda mataji yote ya ndani, kucheza mechi 49 pasipo kupoteza mchezo na kufika fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika (CAF CC), kunaiweka Yanga katika nafasi kushinda tuzo hiyo
Kwa upande wa timu za Taifa, Tanzania pia inawania tuzo ya timu bora ya Taifa ya mwaka barani Afrika
Stars ilifuzu fainali za Afcon 2023 ikiwa mara ya tatu katika hostoria yake




