Kampuni ya Serengeti Breweries Limited (SBL) kupitia Pilsner Lager, imesaini mkataba wa miaka mitatu kuidhamini klabu ya Simba
Mkataba huo wenyewe thamani ya Tsh Bilioni 1.5, ulisainiwa katika hafla iliyofanyika mapema leo
Mtendaji Mkuu wa Simba Imani Kajula amesema udhamini huo umekuja wakati muafaka na utasaidia katika gharama za uendeshaji wa klabu
"Ni ubia wa nguvu kabisa, ubia wa Simba wawili. Hii ni package ambayo imekuja wakati mwafaka. Serengeti ni mbia mkubwa sana wa mpira wa Tanzania, huu ni mwendelezo wa kusaidia mpira"
"Udhamini huu utasaidia uendeshaji wa klabu, gharama za uendeshaji wa vilabu huwa ni kubwa. Upatikanaji wa fedha ni muhimu sana. Tunawashukuru kukubali kuungana nasi kama wadhamini wa Simba," alisema Kajula
Nae Meneja wa Masoko wa SBL, Anitha Rwehumbiza amesema ushirikiano huo utaifanya Serengeti ishiriki matukio mbalimbali ya Simba kuanzia mchezo wa dabi dhidi ya Yanga siku ya Jumapili na mechi nyingine zitakazopigwa Dar es salaam na nje ya Dar es salaam
"Tulikuwa na lengo la kupata mshirika ambaye ana mashabiki wengi, na tulikuwa na furaha tulipopata taarifa kwamba Simba ipo tayari"
"Ukiacha kwamba Simba na Pilsner zinaendana kwa rangi na Simba pia Nguvu Moja ya Simba ni ya kuunganisha Watanzania wote na kinywaji chao cha Pilsner Lager."
"Tutaanza kushiriki matukio ya Simba kwa kuanzia na derby na hata michezo za nje ya Dar. Kwetu ilikuwa na ndoto lakini tunafurahi tumekuja kwa muda sahihi. Tutatumia watu wa vyombo vya habari na tutakuwepo uwanjani kuitangaza Pilsner Lager na Simba," alisema






