Transfer - International

Tetesi za soka Ulaya Ijumaa, Novemba 03 2023

Joel JJ By Joel JJ
β€’
3 Nov 2023
Tetesi za soka Ulaya Ijumaa, Novemba 03 2023

Real Madrid wanamtaka nahodha wa Chelsea Reece James lakini The Blues watadai ada kubwa kwa beki huyo wa England mwenye umri wa miaka 23. (Teamtalk)

AC Milan wana nia ya kumsajili beki Mwingereza Lloyd Kelly mwenye umri wa miaka 25 kutoka Bournemouth, ingawa Tottenham pia wanamnyatia. (Tuttosport - usajili unahitajika, kwa Kiitaliano)

Juventus, Borussia Dortmund, Fulham na West Ham United ni miongoni mwa klabu zingine zinazomtaka Kelly, ambaye mkataba wake unaisha msimu ujao. (90 min)

Arsenal huenda wakamnunua kiungo wa kati wa Royal Antwerp Arthur Vermeeren kwa pauni milioni 13 mwezi Januari, lakini Barcelona pia wanamtaka mchezaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 18. (Sport - kwa Kihispania)

Manchester United wanatafuta mbadala wa kocha Erik ten Hag, huku meneja wa Sporting Lisbon Ruben Amorim na mkufunzi wa zamani wa Real Madrid Zinedine Zidane wakipigiwa upatu kuchukua nafasi yake. (Times - usajili unahitajika)

Manchester United wanataka kumsajili mshambuliaji mwingine ili kumuunga mkono Mdenmark Rasmus Hojlund huku wasiwasi ukiongezeka kuhusu maendeleo ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20. (Mail)

Ivan Toney wa Brentford ni chaguo mojawapo linaloangaliwa na Ten Hag, pamoja na mshambuliaji wa Napoli na Nigeria Victor Osimhen, 24, na mshambuliaji wa Iran na Porto Mehdi Taremi, 31. (Express)

Mshambuliaji wa Uingereza Toney ameithibitishia Brentford kwamba angependa kuondoka mara tu dirisha la usajili la Januari litakapofunguliwa, huku Arsenal na Chelsea wakiripotiwa kutaka kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27. (90min)

Everton wako kwenye mazungumzo na Tottenham kuhusu kubadilisha makubaliano ya uhamisho wa kiungo wa Uingereza Dele Alli, 27. Watakuwa na deni la Spurs la pauni milioni 10 ikiwa Alli atacheza mechi saba zaidi. (Mirror)

Manchester United wanaweza kumnunua kipa wa Porto na Ureno Diogo Costa, 24, huku Andre Onana wa Cameroon akitarajiwa akashiriki Kombe la Mataifa ya Afrika. (Todo Fichajes - kwa Kihispania)

Mshambuliaji wa England Eberechi Eze, 25, ataongeza mshahara wake mara tatu kwa kandarasi mpya ya Crystal Palace ambayo itakuwa na kipengele kikubwa cha kuachiwa. (Teamtalk)

Beki wa Aston Villa na Uhispania Pau Torres, 26, anasema alikuwa karibu kujiunga na Real Madrid kutoka klabu ya zamani ya Villarreal msimu wa 2021. (Sky Sports).

Barcelona wana nia ya kumsajili kiungo wa kati wa Bayern Munich na Ujerumani Joshua Kimmich huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 akiwa hana matumaini kusaini mkataba mpya na klabu hiyo ya Ujerumani. (Fichajes - kwa Kihispania)

BBC

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
7h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
7h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
8h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
11h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
14h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
15h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
16h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
16h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
17h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
18h ago
READ MORE β†’