Klabu ya Wydad Casablanca imetangaza kufariki dunia kwa beki wake wa kushoto, Oussama Faloh (24) ambapo kifo chake kilitokea hapo jana akiwa hospitalini akipatiwa matibabu
Faloh alisajiliwa na Wydad Casablanca dirisha kubwa la usajili lililopita akitokea Klabu ya Angers inayoshiriki Ligi Kuu Nchini Ufaransa
Alipata ajali ya gari wiki tatu zilizopita, ajali hiyo iliyompelekea kupararaizi kisha kupelekwa hospitali kabla ya umauti kumfika hapo jana
Hii ni habari ya kuhuzunisha kwa Wydad ambao bado walikuwa wakisherehekea mafanikio ya kutinga fainali ya michuano ya African Football League baada ya ushindi wa mikwaju ya penato 5-4 dhidi ya Esperance



