Simba - Local

Robertinho kuikabili Yanga kivingine

Joel JJ By Joel JJ
4 Nov 2023
Robertinho kuikabili Yanga kivingine

Kocha Mkuu wa Simba Robertinho Oliveira amesema kikosi chake kinazihitaji alama zote tatu katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Yanga ambao utapigwa kesho Jumapili kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa

Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari mapema leo, Robertinho amesema anatambua mchezo huo hautakuwa mwepesi kwa sababu ni derby lakini jambo muhimu kwa kikosi chake ni kucheza vizuri na kupata ushindi

"Falsafa yangu kwenye mpira wa miguu ni kucheza vizuri na kushinda mechi, Nawaheshimu Yanga ni timu nzuri, lakini nina imani kubwa na wachezaji wetu pamoja na maandalizi mazuri tuliyofanya"

"Mechi ya Derby siku zote haitabiriki. Derby inaamuliwa baada ya dakika 90 za mchezo, tunaiheshimu Yanga lakini tutaingia kwenye mchezo kwa lengo la kutafuta pointi tatu"

"Ninawaamini wachezaji wangu, wana vipaji vikubwa na tumejipanga kushinda. Sina presha ya mechi ya kesho, ni kama michezo mingine lakini kupata pointi tatu ndicho kipaumbele chetu," alisema Robertinho

Simba inazihitaji alama tatu za mchezo dhidi ya Yanga ili kujiweka katika nafsi nzuri zaidi kwenye mbio za ubingwa

Kimahesabu Simba ina nafasi ya kuongoza ligi kwa tofauti ya alama sita kama itashinda mchezo dhidi ya Yanga kesho na mchezo wa kiporo dhidi ya Mashujaa

More Stories

SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa  Yanga SC “Your next: Yanga”
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa Yanga SC “Your next: Yanga”
24m ago
READ MORE →
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
2h ago
READ MORE →
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
12h ago
READ MORE →
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
12h ago
READ MORE →
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
13h ago
READ MORE →
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
16h ago
READ MORE →
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
20h ago
READ MORE →
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
20h ago
READ MORE →
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
21h ago
READ MORE →
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
21h ago
READ MORE →