Tetesi za soka Ulaya, Jumamosi, Novemba 04 2023

Joel JJ By Joel JJ β€’ 4th November 2023


Tetesi za soka Ulaya, Jumamosi, Novemba 04 2023

Sherehe ya kuadhimisha siku ya kuzaliwa ya Marcus Rashford saa chache baada ya Manchester United kushindwa 3-0 na Manchester City "haikubaliki" na fowadi huyo ameomba radhi, anasema meneja Erik ten Hag

Sherehe ya Jumapili iliyopita usiku ilipangwa mapema, na kuhudhuria hafla hiyo haukumzuia Rashford kuwasili kwa wakati kwa mazoezi Jumatatu.

Portland Timbers wako kwenye mazungumzo ya juu zaidi ya kumwajiri beki wa zamani wa Uingereza Phil Neville, 46, kama kocha wao mkuu. Hapo awali alikuwa akiiongoza Inter Miami. (Athletic)

Vilabu kadhaa vya Saudia ikiwa ni pamoja na Al-Nassr vinatamani kumsajili beki wa kati wa Manchester United Mfaransa Raphael Varane, 30, katika dirisha la uhamisho la Januari.(Teamtalk)

Nice wamemwambia beki wa kati wa Ufaransa Jean-Clair Todibo, 23, wako tayari kumuuza mwishoni mwa msimu huu. Manchester United, Arsenal, Tottenham, Newcastle, Bayern Munich, Borussia Dortmund, Bayer Leverkusen, AC Milan na Atalanta zote zinammezea mate (90min)

Inter Miami wamekubali mkataba na mshambuliaji wa Gremio na Uruguay Luis Suarez, 36, ambapo ataungana na wachezaji wenzake kadhaa wa zamani wa Barcelona akiwemo Lionel Messi. (ESPN)

Kiungo wa kati wa Uhispania Thiago Alcantara, 32, anatarajiwa kuondoka Liverpool mkataba wake utakapokamilika mwishoni mwa msimu huu.. (Football Insider) Manchester City inamtaka kiungo wa kati wa Manchester United Muingereza Kobbie Mainoo, 18. (FourFourTwo)

Newcastle wanavutiwa na kiungo wa kati wa Atalanta na Uholanzi Teun Koopmeiners, 25, na beki wa kati wa Genoa na Romania Radu Dragusin, 21 (Gazzetta dello Sport - kwa kiitaliano)

BBC


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.