Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amewapongeza wachezaji wake kwa ushindi mnono wa mabao 5-1 dhidi ya Simba katika mchezo wa ligi kuu ya NBC uliopigwa uwanja wa Benjamn Mkapa
Gamondi amesema huu ni ushindi bora zaidi aliowahi kupata katika maisha yake ya ukufunzi wa mpira wa miguu
"Tulifunga bao la uongozi na kuruhusu bao la kichwa kwenye kipindi cha kwanza, tulikosa umakini. Wakati wa mapumziko niliwaambia wachezaji wangu tunapaswa kuongeza umakini na tujiamini, tucheze soka letu pasipo kuhofia"
"Nimefurahishwa na kile walichofanya kwenye kipindi cha pili, tulitawala mchezo na kupata ushindi dhidi ya timu bora"
"Kama tutaendelea kucheza hivi na kujituma, msimu huu tutafanya mambo makubwa sana," alisema Gamondi
Baada ya ushindi huo Gamondi amesema hakuna muda wa kupoteza kwani wanapaswa kuendelea na ari hii ya ushindi katika mchezo unaofuata dhidi ya Coastal Union
Yanga inasafiri kwenda Tanga kuwakabili Wagosi wa Kaya katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Mkwakwani siku ya Jumatano