Transfer - International

Tetesi za soka Ulaya, Jumatano Novemba 08 2023

Joel JJ By Joel JJ
β€’
8 Nov 2023
Tetesi za soka Ulaya, Jumatano Novemba 08 2023

Manchester United wana nia ya kumsajili beki wa kati wa Nice Jean-Clair Todibo, 23, kama mbadala wa mchezaji wa kimataifa Raphael Varane, 30, ambaye anaweza kuelekea Saudi Arabia. (caught offside)

Bournemouth itakataa mbinu zozote za kumnunua mlinzi Lloyd Kelly mwezi Januari, huku Tottenham, Liverpool, Newcastle na AC Milan zikiwa na nia ya kumnunua Mwingereza huyo mwenye umri wa miaka 25. (Teamtalk)

Wakala wa mlinzi wa Manchester United Mbrazil Antony, 23, anasema mteja wake hatarejea katika nchi yake kwa makubaliano ya kubadilishana mshambuliaji mwenye umri wa miaka 27, Gabriel Barbosa kutoka Flamengo. (Jorge Nicola, via Express)

Miamba wa Italia Juventus wanavutiwa na mkataba wa mkopo wa kiungo wa kati wa Uingereza Kalvin Phillips, 27, ambaye anaelekea kuondoka Manchester City mwezi Januari. (Team talk)

Kiungo wa kati wa Liverpool Thiago Alcantara, 32, analengwa na klabu za Serie A, Juventus na Inter Milan, huku mkataba wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Uhispania na Reds ukimalizika mwishoni mwa msimu huu. (Fichajes)

Kiungo wa kati wa Italia Manuel Locatelli, 25, anatazamiwa kusaini mkataba mpya na Juventus hadi Juni 2028. (Fabrizio Romano)

Chelsea na Liverpool wana nia ya kumsajili mlinzi wa Real Betis mwenye umri wa miaka 18 Assane Diao. (Mucho Deporte, via Football Talk)

Chelsea na Manchester United watalazimika kutumia euro 50m (£43m) kama wanataka kumsajili beki wa kulia wa Uholanzi Denzel Dumfries, 27, kutoka klabu ya Italia Inter Milan. (CalcioMercato)

Arsenal, Fulham na Liverpool zilituma wawakilishi kumtazama kiungo wa Fluminense Andre wakati wa fainali ya Copa Libertadores. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil mwenye umri wa miaka 22 ana makubaliano ya kuondoka kwa mabingwa hao wa Amerika Kusini, ambao thamani yake ni euro 35m (£30.4m) mwezi Januari. (Globo Esporte)

Mlinzi wa Uhispania Marco Alonso, 32, anatarajiwa kuondoka Barcelona na kwenda kwa wapinzani wa La Liga Atletico Madrid. (Football Transfers)

BBC

More Stories

Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
35m ago
READ MORE β†’
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
10h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
11h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
11h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
14h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
18h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
19h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
19h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
20h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
20h ago
READ MORE β†’