Wakati taarifa za ndani kutoka uongozi wa Simba zikibainisha kuwa Bodi ya Wakurugenzi ya klabu hiyo kumtaka Mwenyekiti wa Simba Murtaza Mangungu kujiuzulu nafasi yake, mwenyewe amesema haoni sababu ya kujiuzulu
Jana klabu ya Simba ilitangaza kumfuta kazi aliyekuwa Kocha Mkuu Robertinho Oliveira baada ya kipigo cha mabao 5-1 kutoka kwa Yanga
Ni baada ya Bodi kukutana na kufikia uamuzi huo hhuku ikichukua hatua ya kutaka kuwawajibisha baadhi ya viongozi akiwemo Mangungu
Mangungu amesema Simba inaongozwa kwa mujibu wa taratibu hivyo hatajiuzulu
"Bodi imefikia uamuzi huo sio mimi. Simba inaongozwa kwa mujibu wa utaratibu. Nijiuzulu kwa sababu gani, kwani timu inafanya vibaya? Tumeporeza mechi moja tu, kwa nini hawakusema nijiuzulu wakati tunashinda mfululizo?, " alihoji Mangungu
Aidha, Mangungu amethibitisha taarifa ya baadhi ya wachezaji kuchunguzwa kwa tuhuma za kuihujumu klabu ya Simba katika mchezo huo
"Kuna taratibu za uchunguzi tunazikamilisha tutawajuza zikikamiika," alisema