Bao la dakika ya 71 lililofungwa na Clement Mzize limeihakikishia Yanga alama tatu muhimu mkoani Tanga katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Coastal Union
Krosi ya Jesus Moloko aliyeingia kipindi cha pili ilitumiwa vyema na Mzize aliyeweka mpira kimiani kwa kichwa
Ilikuwa mechi ngumu, ikumbukwe ni siku tatu tu zimepita tangu Yanga ichuane na Simba uwanja wa Benjamin Mkapa na Wananchi kuibuka na ushindi wa mabao 5-1
Ni aina ya mechi ambazo alama tatu ndio matokeo muhimu zaidi ambayo Wananchi watafurahia lakini walipata upinzani kutoka Coastal Union iliyoingia na mkakati wa kujilinda zaidi
Alama 24 kibindoni Yanga ikizidi kupaa kileleni mwa msimamo wa Ligi






