Ili kuepuka migogoro isiyotarajiwa kutoka kwa wachezaji, uongozi wa klabu ya Simba umeleta mapendekezo ya utaratibu mpya wa bonus za wachezaji
Hivi karibuni kumekuwa na taarifa za wachezaji kuendesha migomo ya chini chini kwa kinachoelezwa madai ya malimbikizo ya bonus
Kwa miaka mingi, Simba imekuwa na utaratibu wa kutoa bonus kwa wachezaji pale timu inaposhinda na wakati mwingine bonus huongezeka kulingana na mashindano
Lakini utaratibu mpya uliopendekezwa ni kuwa bonus zitatolewa kwa kuzingatia mafanikio ambayo timu imefikia
Mfano kama malengo ni kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu basi bonus itawekwa kwenye mkataba wa mchezaji na sio utaratibu wa sasa ambapo bonus inatolewa kwa kila ushindi pasipo kujali malengo yamefikiwa mwishoni mwa msimu au la
Kama malengo ni kucheza nusu fainali ligi ya mabingwa basi bonus itafahamika tangu mwanzo wa msimu na itatolewa baada malengo kufikiwa
Wachezaji wanaweza kupewa bonus ambazo ziko nje ya utaratibu huo lakini hizi zinakuwa kama zawadi tu kutoka kwa mabosi



