Yanga kunywa supu Jangwani leo

Joel JJ By Joel JJ β€’ 12th November 2023


Yanga kunywa supu Jangwani leo

Mashabiki na Wanachama wa Klabu ya Yanga leo wameitwa kwenda katika Ofisi za Makao Makuu ya Klabu hiyo zilizopo Mtaa wa Twiga na Jangwani, Kariakoo jijini Dar es salaam kwa ajili ya kunywa supu kusherehekea ushindi wa bao 5-1 walizomfunga mtani wao Simba SC Jumapili iliyopita katika Dimba la Mkapa.

Afisa Habari Yanga SC, Ally Kamwe amesema ng'ombe 10 watachinjwa jangwani leo na Wananchi kunywa supu kufurahia ushindi wao

"Tuna ng'ombe 10, tumepewa kama zawadi. Wanayanga tukutane Jangwani (Makao Makuu ya Yanga), Jumapili asubuhi kunywa supu. Tutachinja ng'ombe, tutakunywa supu"

"Kila mwanayanga atoke nyumbani na maandazi, chapati, vitumbua, mikate, supu ataikuta Jangwani," alisema Kamwe


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.