Mamelodi Sundowns mabingwa AFL

Joel JJ By Joel JJ β€’ 12th November 2023


Mamelodi Sundowns mabingwa AFL

Klabu ya Mamelodi Sundowns imekuwa bingwa wa michuano ya African Football League (AFL) 2023 ikiwa ni mara ya kwanza kufanyika kwake

Mamelodi imeshinda kwa ushindi wa jumla wa mabao 3-2 katika fainali iliyoanza kuchezwa Novemba 5 Morocco na wenyeji Wydad kushinda 2-1 na leo Novemba 12 imefikia tamati kwa Mamelodi kushinda 2-0 na kujihakikishia kitita cha Sh9.9 bilioni

Michuano hiyo ilizinduliwa Oktoba 20 jijini Dar es Salaam kwa mechi ya Simba vs Al Ahly

Timu zilizoshiriki ni Simba, TP Mazembe, Al Ahly, Wydad Casablanca, Enyimba, Esperance, Petroleos de Luanda na Mamelodi Sundowns

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi klabu ya Simba Salim Abdallah 'Try Again' ni miongoni mwa wageni mashuhuri walioshuhudia hitimisho la michuano hiyo


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.