Azam FC itasafiri nchini Kenya ambapo inatarajia kucheza mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Kenya (FKF-PL), Gor Mahia, jijini Nairobi, Novemba 19
Azam inakwenda kucheza mechi hiyo ikiwa ni moja ya maandalizi ya mchezo ujao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mtibwa Sugar utakaochezwa Novemba 24, kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam
Ofisa Habari wa Azam FC, Thabit Zacharia 'Zaka Zakazi’' ametaja sababu ya timu hiyo kusafiri nchini Kenya
"Unajua timu zote ambazo tungetaka kucheza nazo hapa ni zilezile tunazokutana nazo kwenye ligi, hivyo kusingekuwepo na tofauti yoyote ndiyo maana tumeona tucheze na Gor Mahia mechi ambayo itakuwa na tofauti kubwa"
"Timu itaondoka Novemba 18, siku itakayofuata tutacheza mechi na baada ya mechi tutarudi (nchini) kuendelea na maandalizi ya mwisho ya kucheza na Mtibwa Sugar," alisema



