Simba - Local - Transfer

Sven asubiri simu ya mabosi Simba

Joel JJ By Joel JJ
β€’
15 Nov 2023
Sven asubiri simu ya mabosi Simba

Kocha wa zamani wa Simba Sven Vandenbroeck amesema yuko tayari kuchukua majukumu yaliyoachwa na Robertinho Oliveira

Sven aliyeinoa Simba misimu miwili iliyopita na kuisaidia kushinda mataji yote ya ndani na kuipeleka hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa, ametoa kauli hiyo katika mahojiano maalum na mtandao wa  iDiski Times, Afrika Kusini

Sven amesema anaifahamu vyema Simba na anafahamu utamaduni wa klabu, ari ya mashabiki ambao wanaipenda sana klabu yao

Aidha Sven akaeleza sababu ya kutodumu katika klabu alizozifundisha nchini Morocco na Algeria sasa akiwa hana timu

"Kimsingi niko tayari kurejea tanzania kuifundisha Simba, naijua klabu ya Simba na mazingira yake, wana mashabiki wengi wenye mapenzi na timu yao"

"Pale Wydad nilisaini miezi minne kwa sharti la kubeba ubingwa wa Afrika tukapoteza kwa Ahly, CR Belouizdad ni tofauti nilikataa kupangiwa timu na viongozi," alisema Sven

Moja ya sifa yaker kubwa ni msimamo na nidhamu ya kazi, pengine anaweza kuwa kocha sahihi wa kikosi hiki ambacho baadhi ya wachezaji wanatupiwa lawama kuwa hawajitumi

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
7h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
7h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
7h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
11h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
14h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
15h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
15h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
16h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
17h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
18h ago
READ MORE β†’