Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' kimeondoka nchini leo kuelekea Morocco kwa ajili ya mchezo wa kuwania kufuzu kombe la Dunia 2026 dhidi ya Niger
Mchezo huo utapigwa Morocco Jumamosi, Novemba 18, mji wa Marrakech
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan ametoa ndege maalum ya kuipeleka Stars huko Morocco na kuirejesha nchini baada ya mchezo
Novemba 21 Tanzania inakabiliwa na mchezo mwingine dhidi ya Morocco ambao utapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa