Simba - Asec - Local

Kuzishuhudia Simba vs Asec Mimosas buku tano

Joel JJ By Joel JJ
16 Nov 2023
Kuzishuhudia Simba vs Asec Mimosas buku tano

Kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Asec Mimosas utakaopigwa Novemba 25 katika uwanja wa Benjamin Mkapa, Simba imetangaza viingilio vya mchezo huo

Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari, Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ally amesema wameweka viingilio rafiki ili kuhakikisha Wanamsimbazi wanajitokeza kwa wingi kuishangilia timu yao katika mchezo muhimu

"Leo tunazungumzia maandalizi ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya ASEC Mimosas. Utachezwa siku ya Novemba 25, 2023 saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa Mkapa. Wageni watawasili Novemba 23, 2023 wakiwa na msafara wa watu 31. Waamuzi wa mchezo watatoka nchini Misri."

"Viingilio vya mchezo huu ni; Mzunguko - Tsh. 5,000. VIP C - Tsh. 10,000. VIP B - Tsh. 20,000. VIP A - Tsh. 30,000 na Platinum - Tsh. 150,000"

"Wageni rasmi wa mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya ASEC Mimosas watakuwa ni mashabiki wa Simba. Kwanza wametoka kushinda tuzo ya mashabiki bora hivyo kila Mwanasimba akija siku hiyo ajue yeye ni mgeni rasmi."

"Tusahau yaliyopita na tuangalie mbele. Huu ni mchezo wa Ligi ya Mabingwa tukipoteza na tukiwa nyumbani hatutakuwa kwenye sehemu nzuri ya kwenda hatua ya mbele. Twendeni tukawape moyo wachezaji wetu kwamba tunaanguka pamoja na kusimama pamoja," alisema Ahmed

Ahmed amesema kikosi kinaendelea na mazoezi Mo Simba Arena kujiandaa na mchezo huo huku akibainisha kuwa uongozi uko katika hatua za mwisho kukamilisha mchakato wa kocha mpya

"Kikosi kipo mazoezini kuanzia siku ya Jumatatu. Mazoezi yanawahusu wachezaji wote ambao hawana majukumu ya timu za taifa. Ambao wapo kwenye timu za taifa watajiunga na wenzao wakitoka huko. Kikosi bado kipo chini ya Kocha Seleman Matola na Dani Cadena. Uongozi unaendelea na jitihada za kutafuta kocha mpya, mchakato utakamilika muda si mrefu"

"Tupo katikati ya mashindano lazima tutafute kocha ambaye yupo active, atakuwa tayari kuanza majukumu ili akifika kazi ianze"

More Stories

SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa  Yanga SC “Your next: Yanga”
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa Yanga SC “Your next: Yanga”
24m ago
READ MORE →
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
2h ago
READ MORE →
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
12h ago
READ MORE →
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
12h ago
READ MORE →
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
13h ago
READ MORE →
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
16h ago
READ MORE →
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
20h ago
READ MORE →
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
20h ago
READ MORE →
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
21h ago
READ MORE →
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
21h ago
READ MORE →