Yanga - Simba - Local

Yanga, Simba zakumbana na adhabu TPLB

Joel JJ By Joel JJ
β€’
17 Nov 2023
Yanga, Simba zakumbana na adhabu TPLB

Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi Kuu ya Bodi ya Ligi imemfungia kiungo wa Yanga Khalid Aucho mechi tatu kwa kosa la kumpiga kiwiko mchezaji wa Coastal Union Ibrahim Ajibu katika mchezo wa ligi kuu

Aucho pia ametozwa faini ya Tsh 500.000/- kutokana na tukio hilo ambalo pia aliadhibiwa uwanjani kwa kupewa kadi ya njano

Klabu ya Yanga imetozwa faini ya Tsh Milioni 5 kwa kosa la kuingia uwanjani kwa kupitia mlango usiokuwa rasmi kwenye mchezo dhidi ya Simba uliomalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa ,mabao 5-1

Kocha Msaidizi Moussa Ndao na mlinda lango Digui Diarra wametozwa faini ya Tsh 500,000/- kutokana na makosa waliyofanya kwenye mchezo huo

Ndao alidaiwa kuwatolea lugha za matusi maafisa wa benchi la ufundi la klabu ya Simba wakati Diarra alidaiwa kushangilia mbele ya benchi la ufundi la Simba

Klabu ya Simba imetozwa faini ya Tsh Milioni 1 kwa kocha la wachezaji wake kuchelewa kutoka nje kwenye vyumba vya kuvalia nguo katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Yanga

Aidha wachezaji Kibu Denis na Hennock Inonga wametozwa faini ya Tsh 500,000/- kila mmoja wakidaiwa kushangilia bao la Simba kinyume na taratibu

Kibu aliyefunga bao la Simba, alishangilia mbele ya jukwaa la mashabiki wa Yanga huku akitumia ishara ya kuwaziba midomo huku Inonga akidaiwa kushangilia mbele ya benchi la ufundi la Yanga

kamati hiyo pia imewafungia miezi sita mashabiki wanne wa Simba wanaodaiwa kumshambulia shabiki wa Yanga kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Ihefu Fc

More Stories

Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
1h ago
READ MORE β†’
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
11h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
11h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
12h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
15h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
19h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
19h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
20h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
20h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
21h ago
READ MORE β†’