Transfer - International

Tetesi za soka Ulaya, Jumapili Novemba 19 2023

Joel JJ By Joel JJ
β€’
19 Nov 2023
Tetesi za soka Ulaya, Jumapili Novemba 19 2023

Mlindalango wa zamani wa Uhispania David de Gea, 33, amekataa mkataba wa pauni 500,000 kwa wiki na fursa ya kuunganishwa tena na mchezaji mwenzake wa zamani wa Manchester United Cristiano Ronaldo katika klabu ya Saudia ya Al-Nassr . (Sun)

Inter Miami ni moja ya klabu zinazompa De Gea fursa ya kurejea kwenye soka lake huku akiwa hana klabu baada ya kuondoka Manchester United msimu uliopita. (Star)

West Ham wameungana na Newcastle katika kinyang'anyiro cha kumnunua Kalvin Phillips, huku Manchester City wakiwa tayari kumruhusu kiungo huyo wa kati wa Uingereza, mwenye umri wa miaka 27, kuondoka kwa mkopo au kwa mkataba wa kudumu mwezi Januari. (Football Insider)

Fulham wana uwezekano wa kutafuta chaguo lingine kabla ya kufikiria uwezekano wa kumnunua mshambuliaji wa RB Leizpig na Ujerumani Timo Werner, mwenye umri wa miaka 27, mwezi Januari. (Football Insider)

Kiungo wa kati wa Croatia Luka Modric, 38, ameamua kuhamia Saudi Pro League wakati mkataba wake na Real Madrid utakapokamilika msimu ujao. (Sport - in Spanish) Newcastle United wanajaribu kumnunua mshambuliaji wa Stuttgart kutoka Guinea, Serhou Guirassy, 27. (Football Insider)

West Ham wanatazamia kufufua tena azma yao ya kumnunua mshambuliaji wa Bournemouth Muingereza Dominic Solanke, 26. (Mirror)

Tottenham , Aston Villa , Newcastle , Brighton , Brentford na West Ham ni miongoni mwa vklabu zinazomfuatilia kwa karibu kiungo wa kati wa Motherwell mwenye umri wa miaka 17 raia wa Uskochi Lennon Miller. (Teamtalk)

Tottenham pia wanamfuatilia kwa karibu kiungo wa Sunderland Jobe Bellingham, mwenye umri wa miaka 18, ambaye ni kaka yake nyota wa Uingereza Jude. (Football Insider)

Mshambulizi wa Tottenham Alejo Veliz analengwa na klabu ya Serie A ya Bologna , huku mshambuliaji huyo wa Argentina mwenye umri wa miaka 20 akiwa ameshindwa kulazimisha mipango ya mkufunzi wa Spurs Ange Postecoglou tangu kuhama kwake kutoka Rosario Central msimu ujao (Calciomercato - in Italian)

Fulham wanapanga kumnunua mshambuliaji kinda wa Club Bruges na Norway Antonio Nusa, 18, mwezi Januari. (Football Insider)

Manchester United wameajiri wakala wa Los Angeles ili kuwasaidia katika ajira ya 'kukagua vipaji vinavyochipukia'. (Sun)

Everton wanakabiliwa na kulazimishwa kutawala na kupewa adhabu nyingine ya pointi tisa ikiwa klabu pinzani zitafanikiwa kushinda katika madai ya fidia dhidi yao. (Mail)

BBC

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
4h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
5h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
5h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
9h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
12h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
13h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
13h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
14h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
15h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
15h ago
READ MORE β†’