Yanga yahoji adhabu ya Aucho

Joel JJ By Joel JJ β€’ 20th November 2023


Yanga yahoji adhabu ya Aucho

Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga Ali Kamwe amethibitisha klabu hiyo kuandika barua kwa Bodi ya Ligi kuomba ufafanuzi wa adhabu ya kufungiwa mechi tatu aliyopewa kiungo Khalid Aucho

Kamwe amesema Yanga imeomba kupewa ufafanuzi wa adhabu hiyo kwa kuzingatia kuwa kuna wachezaji wa Yanga ambao waliwahi kufanyiwa matukio yasiyo ya kiungwana na klabu iliwahi kulalamika kwa Bodi kuomba hatua zichukuliwe

"Kimsingi hatujakata rufaa adhabu ya kufungiwa mechi tatu aliyopewa mchezaji wetu Khalid Aucho bali tumeandika barua kwa Bodi kuomba ufafanuzi ni kanuni ipi imetumika kumuadhibu Aucho licha ya kuwa tayari alishaadhibiwa uwanjani"

"Wachezaji wetu waliwahi kufanyiwa matukio yasiyo ya kiungwana na tuliandika barua kwa Bodi ya Ligi kuomba hatua zichukuliwe lakini tulielezwa kuwa Kamati haiwezi kutoa adhabu mara mbili kwa matukio ambao mwamuzi aliyaona na kuyachukulia hatua uwanjani"

"Sasa tumeomba tupewe maelezo tofauti kati ya tukio alilofanya Aucho (mwamuzi alimuonyesha kadi ya njano) na mengine ambayo hazikuchukuliwa hatua zaidi baada ya waamuzi kutoa kadi uwanjani," alisema Kamwe


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.