Ijumaa Novemba 24 2023, saa 4 usiku Yanga itakuwa ugenini huko Algeria kuikabili CR Belouizdad katika mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ligi ya mabingwa barani Afrika
Yanga imeondoka nchini Alfajiri ya kuamkia leo Jumanne kuelekea Algeria tayari kwa mchezo huo
Msafara ulioondoka leo, utajumuisha wachezaji ambao hawakuwa na majukumu ya timu za Taifa na kufuatiwa na msafara wa pili ambao utajumuisha wachezaji walio katika timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars'
Msafara huo utaondoka baada ya mchezo wa kuwania kufuzu kombe la Dunia kati ya Tanzania dhidi ya Morocco utakaopigwa leo Jumanne saa nne usiku
Wachezaji wengine Djigui Diarra, Khalid Aucho na Stephane Aziz Ki wanatarajiwa kuungana na kikosi cha Yanga huko Algeria
ADVERTISE HERE