Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetoa taarifa ya klabu ya Simba kufungiwa kusajili na FIFA mpaka pale itakapolipa madai ya klabu ya Teungueth ya Senegal iliyokuwa ikimmiliki mchezaji Pape Ousmane Sakho kabla ya kusajiliwa na Simba
Taarifa iliyotolewa na TFF mapema leo imebainisha kuwa uamuzi huo umefanywa na FIFA baada ya Teungueth kushinda kesi ya madai dhidi ya Simba kutokana na mauzo ya Sakho




