Manula nje mechi dhidi ya Asec Mimosas

Joel JJ By Joel JJ β€’ 24th November 2023


Manula nje mechi dhidi ya Asec Mimosas

Kaimu Kocha Mkuu wa Simba Daniel Cadena amesema mlinda lango Aishi Manula ataukosa mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Asec Mimosas utakaopigwa kesho Jumamosi katika uwanja wa Benjamin Mkapa

Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari mapema leo, Cadena alisema Manula alipata maumivu ya mguu wakati akiwa kwenye majukumu ya timu ya Taifa

Cadena amesema kiungo Clatous Chama alirejea nchini jana akitokea Zambia kwenye majukumu ya timu za Taifa hivyo baada ya mazoezi ya mwisho leo itafahamika kama ataweza kutumika leo au la

"Manula tutamkosa katika mchezo wa kesho kwakuwa ana majeraha,Clatous Chama amewasili jana akitokea Zambia,tutaona kama itawezekana kumtumia dhidi ya Asec Mimosas," alisema

Cadena amesema kikosi chake kiko tayari kwa mchezo huo malengo yakiwa kushinda. Awetaka mashabiki kujitokeza kwa wingi kuwaongezea hamasa wachezaji


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.