Ni rasmi, Simba imemtambulisha Abdelhak Benchikha kuchukua nafasi ya Robertinho Oliveira
Hii ni taarifa iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki wa Simba, hatimaye kocha ametua
Benchikha anatua Simba baada ya kuachana na USM Alger aliyoisaidia kutwaa kombe la Shirikisho barani Afrika (CAF CC) msimu uliopita na Super Cup kwa ushindi dhidi ya Al Ahly
Hakuna shaka Wanasimba wanasubiri kwa hamu kuona vile atarejesha furaha ya Wanamsimbazi
Kesho atakuwa jukwaani dimba la Mkapa kuishuhudia Simba ikiumana na Asec Mimosas