Yanga imeacha alama zote tatu nchini Algeria baada ya kukubali kipigo cha mabao 3-0 dhidi ya CR Belouizdad katika mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ligi ya mabingwa barani Afrika
Yanga iliruhusu mabao mawili kwenye kipindi cha kwanza na kuruhusu bao jingine katika kipindi cha pili dakika za majeruhi
Ulikuwa ni mchezo ambao Yanga ilitawala kwa muda mwingi lakini ilikuwa ngumu kuipenye ngome ya Belouizdad ambao walicheza kwa tahadhari kubwa na kutumia mashambulizi ya kushitukiza
Yanga sasa inarejea nyumbani kujipanga na mchezo unaofuata dhidi ya Al Ahly utakaopigwa Disemba 02