Simba - Local

Simba kuikabili Asec Mimosas ligi ya mabingwa leo

Joel JJ By Joel JJ
25 Nov 2023
Simba kuikabili Asec Mimosas ligi ya mabingwa leo

Simba inaanza kampeni ya hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa barani Afrika kwa mchezo dhidi ya Asec Mimosas ambao utapigwa saa 10 jioni katika uwanja wa Benjamin Mkapa

Kueleka mchezo huo, jana usiku Wanamsimbazi wakapokea taarifa njema baada ya Kocha Abdelhak Benchikha kutangwa kuwa kocha mkuu akichukua nafasi ya Robertinho Oliveira aliyetimuliwa mwanzoni mwa mwezi huu

Huu ni mchezo muhimu kwa Simba kuanza vyema kampeni ya kuisaka nusu fainali ya ligi ya mabingwa

Rekodi zinaibabe Simba, kwani katika misimu minne mfululizo imeweza kutinga robo fainali huku ikitumia vyema uwanja wa nyumbani

Silaha kubwa ya Simba katika mechi hizi ni mashabiki wake, bila shaka wengi watajitokeza kuishangilia timu yao hasa baada ya uongozi kumtangaza kocha mpya

Rais wa heshima klabu ya Simba Bilionea Mohammed Dewji 'Mo' alipunguza bei ya viingilio Mzunguuko ambapo ni Tsh 3,000/- badala ya Tsh 5,000/- ya awali

Ni wazi hautakuwa mchezo mwepesi lakini kwa wachezaji wa Simba hii inapaswa kuwa nafasi yao kuonyesha kilichotokea mechi mbili zilizopita ni upepo mbaya tu ambao ulipita

Ushindi dhidi ya Asec leo utarejesha ari na morali ya Simba katika msimu ambao Wanamsimbazi wanataka kuona mataji yakirejea Mtaa wa Msimbazi

More Stories

BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
50m ago
READ MORE →
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
1h ago
READ MORE →
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
2h ago
READ MORE →
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
2h ago
READ MORE →
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
2h ago
READ MORE →
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
2h ago
READ MORE →
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa  Yanga SC “Your next: Yanga”
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa Yanga SC “Your next: Yanga”
3h ago
READ MORE →
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
4h ago
READ MORE →
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
14h ago
READ MORE →
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
15h ago
READ MORE →