Simba yalazimishwa sare dhidi ya Asec Mimosas

Joel JJ By Joel JJ β€’ 25th November 2023


Simba yalazimishwa sare dhidi ya Asec Mimosas

Mchezo wa Ligi ya Mabingwa kati ya Simba dhidi ya Asec Mimosas umemalizika kwa matokeo ya sare ya bao 1-1

Jinamizi la sare katika michuano ya CAF limeendeleza kuiandama Simba msimu huu

Simba ilitangulia kufunga bao la kuongoza kupitia kwa mkwaju wa penati wa Saido Ntibazonkiza kwenye kipindi cha kwanza kabla ya Asec kurejea katika kipindi cha pili wakiwa bora na kufanikiwa kusawazisha bao hilo

Yatasemwa mengi lakini ni wazi Simba inamuhitaji mtaalam wa 'fitness' haraka sana kwani timu 'inakata moto' kwenye kipindi cha pili

Simba ilicheza kwa nidhamu kubwa kwenye kipindi cha kwanza lakini kasi waliyokuja nayo Asec katika kipindi cha pili ilikuwa tatizo kubwa


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.