Yanga - Local

Yanga yazindua Bacca Day Zanzibar

Joel JJ By Joel JJ
27 Nov 2023
Yanga yazindua Bacca Day Zanzibar

Kuelekea mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Al Ahly ambao utapigwa Jumamosi Disemba 02, leo Yanga imefanya tukio la aina yake visiwani Zanzibar kwa kuzindua siku ya BACCA DAY

Akizungumza katika hafla maalum ya uzinduzi wa tukio hilo, Rais wa Yanga Injinia Hersi Said amesema ni mwendelezo wa utamaduni wa Yanga kuwapa thamani wachezaji wao lakini safari hii tukio hili limekwenda mbali zaidi kwa ajili ya manufaa ya nchi

"Tumekuwa na Maxi Day, Aziz Ki Day, wote walipata nafasi ya kutengenezewa thamani katika mechi zilizopita. Tumekutana hapa Zanzibar leo kwa ajili ya mchezaji wetu Ibrahim Bacca"

"Yanga ilimpa nafasi Bacca ya kuonyesha kipaji chake mazoezini na kwa utulivu na uvumilivu ilimchukua miezi kadhaa mpaka kuaminiwa kwenye kikosi cha kwanza"

"Leo tumekutana kuzindua Bacca Day ambayo kilele chake ni Disemba 02 pale uwanja wa Benjamin Mkapa katika mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Al Ahly"

"Tukio hili limekwenda mbali zaidi sio tu kumpa thamani mchezaji wetu, Taasisi kubwa mbili hapa Zanzibar, ZRA na ZIPA zilipelekewa mapendekezo jinsi gani tukio hili linaweza kuwaongezea thamani"

"Taasisi hizo zimeweka fedha kwa ajili ya kudhamini Bacca Day kila Taasisi ikitoa Tsh Milioni 20. Nawapongeza ZIPA na ZRA kwa kuona kwa kiasi  gani Bacca day inaweza kutumika kuwatangaza"

"Leo natangaza rasmi kuzindua Wiki ya Bacca Day ambayo kilele chake ni Disemba 02 pale uwanja wa Benjamin Mkapa," alisema Hersi

Nae Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga Ali Kamwe amesema Disemba 02 itakuwa siku maalum hivyo watakuwa na mtoko maalum

"Kama una msuli wako uliuweka ndani kwa muda mrefu basi Jumamosi ndio siku yake. Vaa jezi yako na msuli wako njoo uwanjani"

"Lakini pia kama una kanzu yako basi vaa njoo nayo siku hiyo kuja kuipa thamani Bacca Day," alisema Kamwe

More Stories

Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa uhuru
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa uhuru
53m ago
READ MORE →
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
57m ago
READ MORE →
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
1h ago
READ MORE →
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
1h ago
READ MORE →
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa  Yanga SC “Your next: Yanga”
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa Yanga SC “Your next: Yanga”
1h ago
READ MORE →
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
3h ago
READ MORE →
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
13h ago
READ MORE →
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
13h ago
READ MORE →
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
14h ago
READ MORE →
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
17h ago
READ MORE →