Yanga yazindua tawi la wasioona

Joel JJ By Joel JJ β€’ 28th November 2023


Yanga yazindua tawi la wasioona

Rais wa Yanga Injinia Hersi Said leo amezindua Tawi la kwanza nchini la Wanachama wasioona la klabu ya Yanga Kinondoni jijini Dar es salaam

Injinia Hersi ameridhia jina lake kutumika kuwa jina la Tawi na atakuwa mlezi wa Tawi hilo

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi, Injinia Hersi alisema ni faraja kwake kuzindua Tawi la kwanza la wasioona na kuwa ni jambo la baraka kwa klabu ya Yanga kuungwa mkono na watu wasioona

"Nimefarijika sana kama Rais wa hii klabu kuzindua tawi la kihistoria kwenye tasnia hii ya michezo, ni baraka kwa klabu kuungwa mkono na ndugu zetu hawa wasio ona, nawahakikishia nitakuwa mlezi wa tawi hili siku zote, asanteni sana na Mungu azidi kuwa jaalia kila lenye heri"

"Nimesikia risala yenu yote ambayo mliyoomba nimeridhia na tunaanza kuyatekeleza rasmi, nafahamu mmeomba Kompyuta, printer maalumu, spika, fimbo za kutembelea na mengine ambayo mmeyaainisha, vile vile nimeridhia tawi hili kutumia jina langu na kuwa mlezi wa tawi hili"

"Jumamosi tuna mchezo dhidi ya Al Ahly, yeyote ambaye atapendezwa kuja uwanjani tutawaandalia usafiri mpaka uwanjani, tiketi zenu zitaandaliwa na mratibu wetu wa mashabiki, nitafurahi sana wote mkifika uwanjani," alisema Hersi


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.