Kuuzwa kwa fowadi wa Misri Mohamed Salah, 31, msimu ujao kunaweza kufungua milango kwa Liverpool kumsajili fowadi wa Ufaransa Kylian Mbappe, 24.. (Team Talk)
Hata hivyo, Mbappe anaendelea kujitolea kikamilifu kwa Paris St-Germain msimu huu na hakuna dalili yoyote kuto Liverpool ya kutaka kumsajili. (Football Transfers)
Mshambulizi wa Argentina Lautaro Martinez anatarajiwa kusaini mkataba mpya na Inter Milan , licha ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 kuhusishwa na Chelsea na Manchester United . (90 Min)
Everton inamfuatilia kiungo wa kati wa Aston Villa Leander Dendoncker wakati dirisha la uhamisho la Januari likikaribia, huku klabu hiyo ya Midlands ikiwa tayari kusikiliza ofa kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji, 28. (Football Insider)
&The Toffees, pamoja na Crystal Palace , pia wanavutiwa na kiungo wa kati wa Leicester City na Ireland Kasey McAteer, 22. (Football Transfers)
Tottenham huenda ikalazimika kukataa ofa kwa kiungo wa Denmark Pierre-Emile Hojbjerg, 28, na kiungo wa kati wa Uingereza Oliver Skipp, 23, huku mchezaji wa kimataifa wa Uruguay Rodrigo Bentancur, 26, akiwa nje hadi Februari kutokana na jeraha la kifundo cha mguu.. (Telegraph - Usajili unahitajika)
AC Milan watajaribu kupunguza matatizo yao ya safu ya ulinzi kwa kujaribu kumsajili beki wa Arsenal na Poland Jakub Kiwior, 23, kwa mkopo mwezi Januari. (Calciomercato - kwa Kiitaliano)
Chelsea iko tayari kumrejesha kiungo wa kati wa Brazil Andrey Santos mwezi Januari, kwani klabu hiyo haijafurahishwa na hali ya sasa ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19 kwa mkopo huko Nottingham Forest(Fabrizio Romano via kupitia X)
Aston Villa wamemtambua kiungo wa kati wa Lens na Ghana Salis Abdul Samed, 23, kama mbadala wa kiungo wa kati wa Brazil Douglas Luiz, 25, iwapo watalazimishwa kumuuza. (Team Talk)
Newcastle United wanavutiwa na mshambuliaji wa Stuttgart na Guinea Serhou Guirassy mwenye umri wa miaka 27 ili kuimarisha safu yao ya ushambuliaji.. (Rudy Galetti kupitia X)
Kocha wa Nottingham Forest Steve Cooper anaungwa mkono kikamilifu na mmiliki wa klabu Evangelos Marinakis, ingawa Mgiriki huyo anataka kuona kuboreka kwa matokeo ya kilabu hiyo. (Telegraph - usajili unahitajika)
BBC