Transfer - International

Tetesi za soka Ijumaa, Disemba 1 2023

Joel JJ By Joel JJ
β€’
1 Dec 2023
Tetesi za soka Ijumaa, Disemba 1 2023

Manchester United wameungana na Manchester City, Chelsea, Bayern Munich, Borussia Dortmund na Real Madrid katika mbio za kumsaka winga wa Palmeiras Mbrazil Estevao Willian, 16. (Teamtalk)

Winga wa Al-Ittihad Jota, 24, anataka kuungana na mkufunzi wake wa zamani wa Celtic Ange Postecoglou katika klabu ya Tottenham, lakini Postecoglou hana uhakika kuhusu uhamisho wa Mreno huyo. (Sun)

Manchester United pia wameungana na Newcastle, Roma na AC Milan katika kinyang'anyiro cha kumnunua mshambuliaji wa Stuttgart na Guinea Serhou Guirassy mwenye umri wa miaka 27. (Foot Mercato - kwa Kifaransa)

Mwekezaji wa Manchester United Sir Jim Ratcliffe anataka timu yake ya kuajiri kuangazia vipaji vya nyumbani. (Mail)

Arsenal wanajadiliana na mlinzi wa Japan Takehiro Tomiyasu kuhusu kandarasi mpya huku mkataba wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 ukitarajiwa kukamilika 2025. (Athletic - usajili unahitajika)

Manchester United wanajadiliana na kuhusu usajili wa beki wa Romania na Genoa Radu Dragusin, 21. (Prosport - wa Kiromania)

Bei ya winga wa Juventus Muingereza Samuel Iling-Junior mwenye umri wa miaka 20 sasa imewekwa kuwa euro milioni18, kutoka euro milioni 20, na Tottenham wanavutiwa na mchezaji huyo. (Calciomercato - kwa Kiitaliano)

Marc Guehi anataka kusalia Crystal Palace hadi usajili wa majira ya kiangazi ili kuongeza nafasi yake ya kujiunga na kikosi cha Uingereza kwa ajili ya Euro 2024. Beki huyo mwenye umri wa miaka 23 ananyatiwa na Manchester United na Newcastle. (90 min)

Khvicha Kvaratskhelia anayesakwa na Chelsea huenda akavutiwa zaidi na kuhamia Real Madrid, kulingana na babake winga wa Napoli na Georgia mwenye umri wa miaka 22. (Geo Team, via Express)

Manchester City wako tayari kuachana na mpango wa kumnunua kiungo wa West Ham na Brazil Lucas Paqueta, 26, ikiwa suluhu kuhusu uchunguzi wa kamari dhidi ya mchezaji huyo haitakuwa imepatikana. (Uhamisho wa Kandanda)

BBC

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
8h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
8h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
8h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
12h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
15h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
16h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
16h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
17h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
18h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
19h ago
READ MORE β†’