Yanga kuifuata Medeama Fc Jumanne

Joel JJ By Joel JJ β€’ 4th December 2023


Yanga kuifuata Medeama Fc Jumanne

Baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Al Ahly katika mchezo uliopigwa Jumamosi ligi ya mabingwa barani Afrika, Yanga inaelekeza nguvu katika mchezo unaofuata dhidi ya Medeama Fc

Ijumaa ya wiki hii Yanga itakuwa ugenini huko Ghana kumenyana na Medeama katika mchezo ambao Yanga inahitaji kusaka ushindi

Kikosi cha Yanga kinatarajiwa kuondoka nchini Jumanne Desemba 5 kuwafuata Medeama tayari kwa mchezo huo utakaopigwa katika dimba la Baba Yara

Yanga wanaianza safari mapema ikiwa ni mkakati wa kupata muda mzuri wa maandalizi na mapumziko ili kuwakabili wenyeji wao Kwa lengo la kupata ushindi ili kufufua matumaini ya safari ya kuelekea robo fainali

Kama Yanga watafanikiwa kupata pointi hizo tatu ugenini watajiweka katika mazingira mazuri kwani watakuwa na mechi mbili za nyumbani dhidi ya Medeama na CR Belouizdad na iwapo watashinda hizo mbili watafikisha pointi 10 zitakazowapa matumaini ya kwenda robo fainali

Wakati Yanga wakiumana na Medeama, mabingwa watetezi Al Ahly watakuwa wakiumana na CR Belouizdad


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.