Klabu ya Ihefu Fc imeachana na kocha wake Raia wa Uganda, Moses Basena kutokana na mwenendo mbovu wa kikosi hicho katika ligi
Kocha huyo aliyejiunga na Ihefu FC mwezi October akichukua nafasi ya Zuberi Katwila mkataba wake umevunjwa mwezi Desemba mara baada ya makubaliano ya pande zote mbili
Basena amekisimamia kikosi hicho katika michezo sita na kikosi hicho kimekosa kuibuka na ushindi katika michezo hiyo