Mjumbe wa Kamati ya Utendaji klabu ya Yanga Rodgers Gumbo amesema malengo yao ni kushinda mchezo dhidi ya Medeama Fc ambao utapigwa kesho Ijumaa huko Ghana
Gumbo ameongoza msafara wa Yanga ambao ulitua Ghana juzi tayari kwa mchezo huo ambao matokeo ya ushindi kwa Yanga yataweka hai matumaini ya kufuzu hatua ya robo fainali
Gumbo amesema mpaka sasa maandalizi yanakwenda vizuri, timu imepata huduma zote muhimu kutoka kwa wenyeji wao, hakuna matukio yoyote ya hujuma ambayo wamekutana nayo
"Tangu tufike hapa Kumasi kila kitu kinakwenda vizuri, tumepata huduma zote muhimu kutoka kwa wenyeji wetu, niseme tu, hatujakutana na matukio yoyote ya hujuma mpaka sasa"
"Kila timu imejipanga kwenye hatua hii ya makundi hivyo tunatarajia mchezo dhidi ya Medeama hapo kesho hautakuwa mwepesi lakini sisi tunajiandaa na nina uhakika tutapata alama tatu," alisema Gumbo
Yanga leo itakamilisha maandalizi ya mwisho katika uwanja wa Baba Yara, ambao mtanange huo utapigwa Ijumaa, saa 10 jioni (saa 1 usiku Dar)