Mnyama Simba Sc yuko mawindoni Morocco ambapo leo majira ya saa 4 usiku atashuka dimbani huko Marrakesh kuikabili Wydad Athletic katika mchezo wa ligi ya mabingwa barani Afrika, raundi ya tatu kundi B
Mchezo mwingine muhimu kwa Simba kuwania alama tatu ili kuweka hai matumaini ya kufuzu robob fainali
Hata hivyo ni mchezo ambao utahitaji wachezaji kujitoa kwa jasho na damu ili kuhakikisha malengo yanatimia
Wydad wamepoteza mechi zote mbili za awali, leo wataingia uwanjani wakiwa na dhamira ya kuzisaka alama tatu katika uwanja wao wa nyumbani
Ni mechi ya kuamua hatma yao, ni wazi utakuwa mchezo wenye presha kubwa lakini Simba ina uzoefu wa mechi za aina hii
Msimu uliopita timu hizi zilikutana hatua ya robo fainali Simba ikiwa na faida ya ushindi wa bao 1-0 waliopata kwenye mchezo wa kwanza
Mchezo ukamalizika kwa Wydad kushinda 1-0 na hivyo changamoto ya mikwaju ya penati ikatumika kuamua mshindi na Wydad kutinga nusu fainali
Kocha Mkuu wa Simba Abdelhak Benchikha ana uzoefu na soka la Morocco hivyo anafahamu ni namna gani leo kikosi chake kinapaswa kucheza ili kuhakikisha hawapotezi mchezo
Simba inahitaji ushindi katika mchezo huo lakini pia hata alama moja itakuwa na faida kuelekea mchezo wa marudiano ambao utapigwa Disemba 19 jijini Dar es salaam



