Ligi Kuu ya NBC inaendelea leo ambapo mechi mbili zinatarajiwa. Singida FG ambayo imehamishia makazi yake Karatu kwa muda kufuatia uwanja wao wa CCM Liti kufungiwa, watakuwa wenyeji wa KMC
Azam Fc ambayo ilishusha vipigo vya 5G katika michezo miwili iliyopita dhidi ya Mtibwa Sugar na KMC, itashuka tena uwanja wa Azam Complex kumenyana na JKT Tanzania katika mchezo utakaopigwa saa 1 usiku
Klabu za Yanga na Simba ambazo zinashiriki hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa, wiki hii zinarejea kwenye mikiki mikiki ya Ligi Kuu ambapo Ijumaa, Disemba 15 Simba itamenyana na Kagera Sugar mchezo utakaopigwa uwanja wa Uhuru wakati Jumamosi Yanga itamenyana na Mtibwa Sugar mchezo utakaopigwa uwanja wa Azam Complex

ADVERTISE HERE