Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imewasilisha malalamiko rasmi kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuwataka Yanga SC kugharamia uharibifu uliofanyika kwenye mchezo wao dhidi ya Al Ahly
Barua ya Wizara inasema, Wizara ilitoa kibali cha kufanyika kwa mchezo wa kimataifa kati ya Yanga SC (Tanzania) dhidi ya Al-Ahly (Misri) katika Uwanja wa Benjamin Mkapa uliofanyika Desemba 2
Hata hivyo, Wizara imepokea Malalamiko kutoka kwa Uongozi wa uwanja ambapo mashabiki wa Yanga SC wanalalamikiwa kwa kuwasha fataki wakati mchezo ukiendelea na kusababisha vurugu zilizopelekea baadhi ya viti kung'olewa
Wizara inakemea vikali kitendo hiki na kuwataka Yanga SC mara moja kuwasiliana na uongozi wa Uwanja ili kubaini ukubwa wa tatizo na kuona namna bora ya kulitatua
Kwa barua hii, Wizara inawasilisha rasmi malalamiko haya kwa TFF kwa kuwa ndiye mdhamini wa vilabu hivi kwa maombi ya matumizi ya uwanja huu ili kuwajulisha Yanga SC kuwa inapaswa kugharamia matengenezo ya viti vilivyong'olewa na mashabiki wakati wa mchezo huu
Aidha kuwaonya mashabiki wao kuacha mara moja tabia hizi ili uendelea kustawisha michezo na kuulinda Uwanja wa Benjamin Mkapa.