Yanga - Local

Yanga yalalamikia waamuzi CAF CL

Joel JJ By Joel JJ
β€’
12 Dec 2023
Yanga yalalamikia waamuzi CAF CL

Baada ya mechi tatu za hatua ya makundi kukamilika, Yanga imekumbana na matukio kutotendewa haki na waamuzi na hivyo kupeleka malalamiko kwa Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) baada ya matukio yaliyojiri kwenye mchezo dhidi ya Medeama

Ukianza na mchezo dhidi CR Belouizdad waamuzi waliwapendelea wenyeji wazi wazi katika matukio mengi ikiwa ni pamoja na kuinyima Yanga mkwaju wa penati baada ya Pacome Zouzoua kuangushwa ndani ya eneo la hatari dakika za mwanzo katika mchezo huo

Kwenye mchezo dhidi ya Al Ahly ambao ulipigwa uwanja wa Benjamin Mkapa kulikuwa na matukio mengi ambayo mwamuzi alionekana kuwa na kigugumizi hasa inapoonekana faida ni kwa upande wa Yanga

Tukio la Pecy Tau kumkanyaga Joyce Lomalisa na kumsababishia maumivu yaliyomfanya ashindwe kuendelea na mchezo ni mfano wa matukio hayo. Mwamuzi hakutoa kadi yoyote katika tukio ambalo Tau angeweza hata kuonyeshwa kadi nyekundu

Mchezo uliofuata dhidi ya Medeama nao haukuwa na tofauti kwenye maamuzi. Achana na rafu mbaya aliyocheza beki Kwadwo Amoako dhidi ya Nickson Kibabage ambayo ilistahili kadi nyekundu ya moja kwa moja, katika mchezo huo Yanga ilinyimwa bao halali kabisa

Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, Rodgers Gumbo amesema wamelazimika kuandika barua ya malalamiko kwa CAF wakimlalamikia yale waliyofanyiwa katika mchezo dhidi ya Medeama

"Ni kweli tumepeleka barua ya malalamiko kwa CAF kutokana na kuwa na ushahidi wa matukio ambayo ni wazi hatukutendewa haki ambayo ni pamoja na rafu ambayo mchezaji wetu Nickson Kibabge alichezewa na mchezaji wa Medeama ambaye alistahili kuonyeshwa kadi nyekundu lakini refa hakufanya hivyo"

"Lakini pia kuna tukio la bao letu halali ambalo Kibabage alifunga lakini refa akalikataa, tumejiridhisha lilikuwa bao halali"

"Tumewaandikia ili wajue nini cha kufanya kwa sababu matukio kama yale yananyima timu haki ya kupata ushindi na kuipa nyingine matokeo ambayo haijastahili," alisema Gumbo

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
1h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
2h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
3h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
5h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
19h ago
READ MORE β†’