Jana Cristiano Ronaldo alipachika goli lake la 50 kwa mwaka huu wa 2023 wakati timu yake Al-Nassr walipowafunga mahasimu wao Al-Shabab kwa magoli 5-2 na kutinga nusu fainali ya Kombe la Mfalme (Saudi King Cup)
Mchezaji huyo wa zamani wa Real Madrid na Manchester United alifunga goli la nne kwenye mchezo huo katika kipindi cha pili
Goli hilo limefikisha magoli 26 katika msimu huu, 16 kati ya hayo yakifungwa katika Ligi Kuu ya Saudia (Saudi Pro League)
Siku chache zilizopita Ronaldo alicheza mechi yake ya 1200 kwenye mchezo dhidi ya Al-Riyadh ambao timu yake ilishinda 4-1. Alifunga goli moja na kutoa ‘assist’ moja kwenye mchezo huo
Ronaldo ndiye mchezaji aliyefunga mabao mengi zaidi kwenye Saudi Pro League msimu huu mpaka sasa