Ni rasmi Simba Queens imetwaa Ngao ya Jamii kwa ushindi wa mikwaju ya penati dhidi ya JKT Queens katika mchezo wa fainali uliopigwa uwanja wa Azam Complex
Dakika 90 za mchezo huo zilimalizika kwa matokeo ya sare ya bao 1-1 na Simba Queens kushinda kwa penati 5-4
Stumai Abdallah alitangulia kuifungia JKT Queens bao la kuongoza kabla ya Dunai Bhobho kuisawazishia Simba Queens
Simba Queens ikaweka kambani mikwaju yote mitano ya penati wakati JKT Queens wakikosa mkwaju mmoja
Ni taji la kwanza kwa Simba Queens msimu huu kama ilivyo kwa kaka zao Simba Sc ambao walitwaa Ngao ya Jamii mkoani Tanga



