Safari ya Manchester United katika ligi ya mabingwa Ulaya msimu huu ilifikia tamati mapema Jumanne usiku baada ya kupoteza nyumbani kwa Bayern Munich na kusababisha vijana wa Erik ten Hag kumaliza mkiani mwa Kundi A
Baada ya kuchukua pointi nne pekee katika mechi tano za mwanzo, United wakihitaji kushinda ili kuwa na nafasi yoyote ya kusalia kwenye michuano hiyo
Lakini kichapo cha 1-0 kiliwafanya The Red Devils kumaliza katika nafasi ya nne kwenye kundi la UCL kwa mara ya kwanza tangu 2005
Hii ilikuwa kampeni mbaya zaidi ya United kwenye Ligi ya Mabingwa kuwahi kutokea
Klabu ya Manchester ilikuwa haijawahi kupata chini ya pointi sita katika hatua ya makundi
United pia iliweka rekodi mbaya ya kufungwa mabao 15 katika michezo yao sita - zaidi ya timu yoyote ya Ligi Kuu iliyowahi kufungwa kwenye kundi la UEFA CL



