Simba - Local

Benchikha abaini mapungufu Simba

Joel JJ By Joel JJ
β€’
13 Dec 2023
Benchikha abaini mapungufu Simba

Baada ya kuiongoza Simba kwa takribani wiki mbili, Kocha Mkuu wa Simba Abdelhak Benchikha amesema kikosi chake kimesheheni wachezaji wengi wenye uwezo mkubwa lakini ipo changamoto katika baadhi ya maeneo hasa safu ya ushambuliaji

Benchikha amesema wanaendelea kufanyia kazi mapungufu hayo na anaamini baada ya muda kila kitu kitakuwa sawa

Benchikha amewasifu nyota wake wanaocheza eneo la kiungo kuwa wanafanya kazi kubwa na kwake ndio eneo lililomvutia zaidi

"Nafikiri tunakwenda vizuri, tuna timu yenye wachezaji wazuri lakini zipo changamoto katika baadhi ya maeneo"

"Nimeridhishwa na vile timu inavyocheza hasa eneo la kiungo, wanafanya kazi nzuri katika kuhakikisha kwamba wanakaba, lakini pia wanapiga pasi za uhakika kwenda mbele na wameonyesha jinsi gani wanataka kuona timu inapata ushindi"

"Ipo changamoto kidogo eneo la ushambuliaji, kwa sababu hatujafunga mabao mengi, ila nafanyia kazi hali hiyo na naamini baada ya muda kila kitu kitakaa sawa," alisema Benchikha

Nyota wanaon'gara katika eneo la kiungo ni Fabrice Ngoma na Sadio Kanoute ambao wamekuwa chaguo la kwanza tangu ujio wa Benchikha wakisaidiana na Mzamiru Yassin ambaye amekuwa akitumika katika kipindi cha pili

Simba imerejea Mo Simba Arena kujiandaa na mchezo unaofuata Ligi Kuu dhidi ya Kagera Sugar ambao utapigwa Ijumaa, Disemba 15 katika uwanja wa Uhuru

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
1h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
1h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
1h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
5h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
8h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
9h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
10h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
10h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
11h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
12h ago
READ MORE β†’