Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi imejadili maombi ya merejeo (review) ya klabu ya Yanga kuhusu adhabu ya kufungiwa michezo mitatu (3) na kutozwa faini ya sh. 500, 000 iliyotolewa kwa mchezaji Khalid Aucho kupitia kikao cha kamati hiyo cha Novemba 14, 2023
Hata hivyo, baada ya kupitia maelezo ya klabu ya Yanga na kanuni za Ligi, kamati imejiridhisha kwa mara nyingine kuwa adhabu iliyotolewa kwa mchezaji huyo ni sahihi hivyo anapaswa kuendelea kuitumikia, huku ikimtaka mchezaji huyo kuzingatia mchezo wa kiungwana wakati wote
Aucho sasa atakosa mechi tatu za ligi zinazofuata akianza na mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar utakaopigwa uwanja wa Azam Complex kesho