Kocha Mkuu wa Simba, Abdelhak Benchikha baada ya kutoka Ligi ya Mabingwa, leo atakuwa na mtihani mwingine kwenye Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar inayonolewa na kocha Meckie Mexime utakaochezwa saa 10:00 jioni katika uwanja wa Uhuru
Benchikha amekaa benchi kwenye mechi mbili za Simba dhidi ya Jwaneng Galaxy 0-0 na Wydad ambayo walifungwa 1-0
Pamoja na Simba haikupata ushindi katika mechi hizo, kuna dalili njema zilionekana za kikosi chake kuimarika kiuchezaji
Pasipo na shaka leo mashabiki wa Simba wanatamani kuona timu yao ikiwa katika ubora na kushinda mchezo wa leo
Mchezo huo utakuwa sehemu ya maandalizi ya Simba kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Wydad utakaopigwa Jumanne