Yanga - Local

Gamondi akerwa na wanaoshinikiza rotation

Joel JJ By Joel JJ
β€’
15 Dec 2023
Gamondi akerwa na wanaoshinikiza rotation

Kocha wa Yanga, Miguel Gamondi amesema watu wengi wanahoji kwanini hatoi nafasi ya wachezaji wengine kupata nafasi kwenye kikosi chake 'Rotation' lakini yeye anajua kwanini anafanya hivyo

Gamondi amesema watu wanaohoji jambo hilo ndio walewale waliozungumza siku alipofanya mabadiliko kwenye mchezo dhidi ya Ihefu mchezo ambao Yanga walitandikwa mabao 2-1 mkoani Mbeya

"Nakumbuka mchezo dhidi ya Ihefu nilifanya ‘Rotation’ nikawapanga akina Diarra, Bakari, Kibwana Moloko, Skudu, Mzize na niwaambie tuu hawa ni wachezaji wakubwa sikupanga timu ya vijana lakini tulifungwa, hatukufungwa kwasababu ya 'Rotation' tulifungwa kwasababu hata msimu uliopita tulifungwa pia," alisema

Kocha huyo ameongeza kuwa haoni sababu ya kufanya mabadiliko ikiwa bado anaendelea kupata ushindi katika michezo ambayo anacheza na atafanya mabadiliko ikiwa yeye na benchi lake la ufundi wataona ipo haja ya kufanya hivyo

Kesho Yanga watashuka dimbani kuwavaa Mtibwa Sugar kwenye muendelezo wa Ligi kuu Tanzania Bara.

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
1h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
1h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
2h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
5h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
9h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
9h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
10h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
10h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
11h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
12h ago
READ MORE β†’