Dirisha dogo la usajili limefunguliwa leo Disemba 16 2023 na linatarajiwa kufungwa Januari 15 2024
Timu zinazoshiriki Ligi Kuu, Championship, First League na Ligi ya Wanawake zitakuwa na nafasi ya kufanya maboresho ya vikosi vyao
TFF imezitaka timu kukamilisha usajili na kupata (ITC) kwa wachezaji kutoka nje ya nchi ndani ya muda kwani hakutakuwa na muda zaidi wa nyongeza pale dirisha litakapofungwa