Yanga - Simba - Azam - Local - Singida

VAR kutumika Ligi Kuu Tanzania

Joel JJ By Joel JJ
β€’
16 Dec 2023
VAR kutumika Ligi Kuu Tanzania

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limebainisha kuwa baadhi ya mechi za Ligi Kuu Bara zitaanza kuamuriwa kwa usaidizi wa teknolojia ya video ya waamuzi (VAR)

Hiyo ni kufuatia uamuzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), kuipa Tanzania vifaa vya VAR ambavyo vitafungwa katika baadhi ya viwanja

Akizungumza katika mkutano mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) unaofanyika Iringa, Rais wa shirikisho hilo amesema , Wallace Karia amesema wanaandaa utaratibu wa ufungwaji wa vifaa hivyo kwa kushirikiana na wadu

"Niwape habari njema kuwa tumepata VAR kutoka CAF na hii ni mwendelezo wa uhusiano mzuri na CAF. Wataalamu wameingia jana kutoa mafunzo. Itafungwa katika viwanja vyenye standard (ubora)"

"Kamati ya waamuzi kwa vile tumewapa jukumu la usimamizi mtasaidia katika mafunzo na uzuri tunaye mkufunzi wa waamuzi wa CAF, Leslie Liunda ambaye atakuwa mratibu wa hayo mafunzo," alisema

Karia amesema kuwa wanaangalia pia uwezekano wa VAR kufungwa katika Uwanja wa Amaan Zanzibar ikiwa ni katika kuhakikisha kwamba mchezo wa soka unaendelea kupata mafanikio hapa nchini

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
44m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
2h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’